User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active
 

Tarehe 30/10/2015, Balozi za nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilizopo Paris Ufaransa ziliadhimisha siku ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo mkazo wake ulikuwa ni kuenzi ; kudumisha ; kukuza ; na kutangaza lugha ya Kiswahili. Shughuli hii ilifanyika katika makazi ya Mhe. Begum K. Taj, Balozi wa Tanzania Ufaransa ambaye ni mwenyekiti wa Mabalozi wa nchi za Jumuiya hii.

Kwa kawaida siku hii inaadhimishwa kila mwaka tarehe 30/11. Lakini, kutokana na umuhimu wa mkutano ujao wa Kimataifa wa Tabia Nchi (COP 21) utakofanyika Paris kuanzia tareh 30/11 – 12/12 Desemba 2015, mabalozi wa nchi hzi waliona ni vyema kuadhimisha siku hii mwezi Octoba ili kupata nafasi nzuri ya kushiriki katika ufunguzi wa COP 21.

Waalikwa zaidi ya 200 walihudhuria hafla hii ambayo ilifanyika kwa lugha ya Kiswahili na ilikuwa na matukio yafutayo :- maonyesho ya khanga, ngoma na maelezo kuhusu umuhimu wa  lugha ya kiswahili yaliyotolewa na wanafunzi wa kifransa wanaosoma kiswahili katika chuo cha INALCO kilichopa Paris. Aidha, kulikuwa na chakula cha jioni kilichoandaliwa balozi za nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili ukuonyesha utamaduni wa chakula wa eneo hili. Shughuli hii ilifana sana.